logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maafa katika mgodi Migori, 2 waaga dunia, 10 wakwama

Watu wawili waaga dunia baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka kule Migori.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 July 2024 - 06:32

Muhtasari


  • •Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo alithibitisha kisa hicho huku akiomba usaidizi katika shughuli ya uokoaji.
  • •Wengine wanne wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo.
crime scene

Watu wawili wamethibitishwa kufariki baada ya ukuta wa mgodi wa dhahabu wa mita 750 kuporomoka huko Kanga, Kaunti ndogo ya Rongo, Migori.

Wachimba migodi 18 walikuwa kazini kwenye mgodi wa dhahabu wa Choppa wakati kuta zilipoporomoka. Zaidi ya watu 10 bado wamekwama katika mgodi huo huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea.

Wengine wanne wanapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo.

Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo George Otenga, watu 18 walikuwa kwenye mgodi huo kabla ya kuporomoka.

Naibu kamishna wa kaunti vile vile alisema kuwa serikali ya kaunti ya Migori imekusanya wafanyikazi na rasilimali kusaidia kuwaokoa wale ambao bado wamekwama ndani ya mgodi huo.

Serikali ya kaunti inasalia na matumaini kuwa itafanikiwa kuwafikia watu walionaswa hivi karibuni.

Tutakuletea taarifa zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved