Mbunge wa Dadaab Farah Maalim amefukuzwa katika hoteli moja mjini Mombasa pwani ya Kenya kufuatia kauli yenye utata aliyotoa hivi karibuni dhidi ya waandamanaji vijana wa Gen Z.
Katika video iliyosambaa kwa kasi mitandaoni mbunge huyo anaonekana akisema ‘’waandanaji walifanya uhaina na laita angelikuwa rais angeliwaua’’
Vyombo vya Habari vya ndani vinaripoti kuwa Mbunge huyoalifika katika hoteli hiyo siku ya Ijumaa.
Mkurugenzi Mkuu wa hoteli hiyo Jimi Kariuki alitoa tangazo la kufukuzwa kwa mbunge huyo katika mtandao wa X zamani Twitter baada ya baadhi ya watumiaji wake kuishtuma kwa kumruhusu kukaa hapo.
Good evening. He is no longer a guest at our hotel. We asked him to leave the hotel earlier in the day. We do not in anyway condone his inflammatory and threatening statements against Kenyans and will not associate our brand with such a person.
— Jimi Kariuki (@KariukiJimi) July 12, 2024
Bw. Kariuki asisitiza kuwa hoteli hiyo haikubaliani kwa vyovyote na kauli ya Maalim.
Katika video hiyo ambayo haijulikani ilirekodiwa lini, Maalim, akizungumza kwa lugha ya Kisomali anaonekana, akisema kuwa kama angekuwa Rais wa Kenya angewaua waandamanaji 5,000 kila siku.
Tafsiri ya video iliyothibitishwa ilifichua kuwa mbunge huyo alikuwa akiwashutumu Vijana wa Kenya kwa jaribio lao la kuandamana hadi Ikulu wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa fedha wa 2024.
Mbunge huyo hata hivyo amekanusha madai hayo akisema video hiyo ilifanyiwa ukarabati.