logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alinur ashatkiwa kwa kuchapisha habari za uongo, aachiliwa kwa dhamana ya Ksh.30,000

Alinur aliwakilishwa na mawakili Sadam Hussein na Asha Bashir.

image

Habari18 July 2024 - 14:25

Muhtasari


  • Mahakama ilisikiliza maelezo hayo kwa uwongo yakimuonyesha Hussein Mohammed, MBS kama mwandishi akitumia akaunti ya X ya mtandao wa kijamii @Husseinmuhamedg, kwa nia ya kwamba data hiyo itachukuliwa kuwa ni ya kweli.

Mwanasiasa Alinur Mohamed Bule ameshtakiwa kwa kuchapisha habari za uongo zinazodai kuwa yeye ni Msemaji wa Ikulu.

Bule alishtakiwa kuwa mnamo Julai 15 mwendo wa saa 1408 kwa kutumia akaunti yake ya X ya mtandao wa kijamii mahali pasipojulikana pamoja na watu wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama, alichapisha data za uongo kimakusudi.

Karatasi ya mashtaka inasema, "Mimi ni mwandishi wa habari niliyegeuzwa kuwa Msemaji wa ikulu, lakini siwezi kustahimili propaganda hii tena. Ni kinyume na maadili yangu kusema uwongo. Ni afadhali kupoteza kazi yangu kuliko kuhatarisha kanuni zangu."

Mahakama ilisikiliza maelezo hayo kwa uwongo yakimuonyesha Hussein Mohammed, MBS kama mwandishi akitumia akaunti ya X ya mtandao wa kijamii @Husseinmuhamedg, kwa nia ya kwamba data hiyo itachukuliwa kuwa ni ya kweli.

Alikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Robinson Ondieki.

Alinur aliwakilishwa na mawakili Sadam Hussein na Asha Bashir.

Aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh30,000.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 1.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved