logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto kuhutubia taifa saa kumi jioni

Hotuba hiyo inajiri huku Wakenya wakitarajia mabadiliko zaidi katika usimamizi wake.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 July 2024 - 11:24

Muhtasari


  • •Hotuba hiyo inakuja baada ya wiki moja baada ya kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wake ambayo yalisababisha makatibu wote wa baraza la mawaziri kurudishwa nyumbani.

Rais William Ruto atahutubia taifa leo saa kumi jioni katika Ikulu ya Nairobi.

Hotuba hiyo inakuja baada ya wiki moja  ya kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wake ambayo yalisababisha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri .

Pia hotuba hio inajiri wakati Wakenya wanatarajia mabadiliko zaidi katika utawala wake kulingana na wasiwasi uliotolewa na Gen Zs.

Rais William Ruto alivunja Baraza lake la Mawaziri na kuwarudisha nyumbani mawaziri wote na mwanasheria mkuu.

Uamuzi huo hauathiri Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.

"Nimeamua kuwafuta kazi mara moja mawaziri na mwanasheria mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya isipokuwa waziri mwenye mamlaka makuu na Katibu wa Baraza la Mawaziri," Ruto alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved