Hassan Mugambi, ambaye ni mshauri wa mawasiliano katika wizara ya ulinzi anaomboleza kifo cha nyanyake.
Habari hizo zilitangazwa na rafiki yake mkubwa Rashid Abdallah,ambaye ni mwanahabari katika runinga ya Citizen. Rashid, alisema ibaada ya mazishi itafanyika Jumanne mchana katika eneo la Kibra.
"Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un . Ndugu yangu @hassanmugambi amefiwa na nyanya mzaa mamake. Mazishi Inshallah ni kesho saa saba mchana Kibra. Pole kwa familia. Nenda salama Ayeyo."
Kwa upande mwingine Mugambi amemtaja bibi yake kuwa ni baraka kubwa katika maisha yake.
"Ulikuwa baraka sana uliyewaongoza watoto wako pamoja na watoto wao ,kumtanguliza mungu siku zote. Ulituombea sana tulitokwa na machozi katika maombi yako. Leo tunakuombea na hatutakoma mpaka Jannah inshallah...Allah akuweke mahali pema peponi."
Mwanahabari Lulu Hassan pia ameonyesha masikitiko baada ya habari hio huku akisema;
"Inna lillahi wa ina illayhi Rajiun ...it is well Kabarsunuu."
Nyanyake Mugambi alizaliwa mwaka wa 1924.