logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mswada wa kudhibiti ubora wa afya kutoa afueni kwa wagonjwa

Dkt. Kigen alitangaza kuwa sheria mpya itahakikisha vituo vya afya vya umma na binafsi nchini vinazingatia viwango vilivyothibitishwa vya utoaji huduma

image
na SAMUEL MAINA

Habari22 July 2024 - 09:40

Muhtasari


  • •Dkt. Kigen Bartilol alitangaza kuwa sheria mpya itahakikisha kwamba vituo vya afya vya umma na binafsi nchini kote vinazingatia viwango vilivyothibitishwa vya utoaji huduma
  • •Dkt. Kigen alisema kuwa watasimamisha taasisi huru kusimamia na kushauri serikali kuhusu masuala ya usalama na ubora katika huduma za afya

Wagonjwa katika hospitali za Kenya watanufaika na viwango vya juu vya huduma za matibabu wakati mswada wa kudhibiti ubora wa afya utapitishwa kuwa sheria.

Mswada huo unaojulikana kama Mswada wa Ubora wa Huduma unatarajiwa kuziba pengo kubwa katika matokeo ya afya na kukuza uboreshaji hospitali za umma na za kibinafsi.

Hii itakuwa mojawapo ya mbinu za kukuza azma ya kufikia idadi sifuri ya vifo vya wagonjwa vinavyoweza kuzuilika.

Akiongea alipokuwa akitoa hotuba kuu katika hafla ya Uongozi ya African Consortium for Quality Improvement Research in Frontline Healthcare (ACQUIRE) Nairobi mnamo Jumatatu, Dkt. Kigen Bartilol alitangaza kuwa sheria mpya itahakikisha kwamba vituo vya afya vya umma na binafsi nchini kote vinazingatia viwango vilivyothibitishwa vya utoaji huduma.

"Itawezesha watoa huduma za afya kutoa tathmini za muundo na mchakato wa vituo vya afya vinavyoshughulikia uwezo wao wa miundombinu, rasilimali watu, na taratibu.

Tunatarajia kuwa wagonjwa watapata huduma bora za afya kote nchini," alieleza, akiongeza kuwa itasimamisha taasisi huru kusimamia na kushauri serikali kuhusu masuala ya usalama na ubora katika huduma za afya, hivyo kuhakikisha ithibati inayotambuliwa kimataifa yenye alama ya ubora.

Dkt. Kigen alisema kuwa Kenya inakabiliwa na mzigo mkubwa wa magonjwa ya kuambukizana na yasiyo ya kuambukizana na kwamba imefikia hatua ambapo uboreshaji ni muhimu katika kufikia azimio la Kujumuisha Kote kwa Huduma za Afya la nchi.

Akitoa maoni yake, Dkt. Lydia Okutoyi alionyesha kuwa kuweka viwango vya ubora katika huduma za wagonjwa ni muhimu kwa kuimarisha mifumo ya afya ya Kenya ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika.

"Mtandao wetu wa afya uko katika hali ya dharura, ukipambana na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi na dawa, operesheni zisizounganishwa za hospitali, kutokuwa na vifaa vya kutosha kushughulikia milipuko na janga pamoja na mtazamo unaozingatia matibabu ya magonjwa badala ya majibu kamili ya mfumo kwa wagonjwa.

Hii inazidishwa na gharama kubwa ya matibabu, uhaba wa vifaa vya kutosha na sahihi, vikwazo vya kisheria, na dawa ghali," alisema.

Dkt. Okutoyi alisema kuwa  Mswada mpya wa Ubora wa Huduma utasaidia kuinua viwango vya huduma za afya nchini kwa kuelekeza rasilimali, ahadi, uwekezaji na uvumilivu na wadau wengi ikiwa ni pamoja na serikali, mameneja wa vituo vya afya, bima za afya na madaktari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved