Maafisa wa upelelezi huko Kuresoi wamemtia mbaroni msaidizi wa chifu kwa madai ya unajisi.
Chifu Msaidizi, 42, anadaiwa kumnajisi msichana huyo wa miaka minne.
Kulingana na taarifa ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mwanamume huyo alikamatwa baada ya wazazi wa mtoto huyo kuripoti kisa hicho.
"Kukamatwa huko kulifuatia ripoti ya kuhuzunisha kutoka kwa wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka 4 ambaye alikuwa amelalamikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuwafanya wazazi wake kuchunguza zaidi," DCI alisema.
DCI alisema mtoto huyo alifichua kuwa alinajisiwa na mshukiwa na kusababisha wazazi hao kumpeleka hospitalini mara moja ili kuchunguzwa na kutibiwa.
DCI ilisema baada ya kupokea ripoti hiyo, uchunguzi wa kisa hicho ulianza na kupelekea mshukiwa kukamatwa.
Mshukiwa huyo amefikishwa mahakamani na kwa sasa amezuiliwa Nakuru.
DCI ilisema kuwa kesi hiyo itatajwa Julai 25, 2024.