Jumatano asubuhi, Rais William Ruto Jumatano alitangaza hadharani orodha yake ya pili ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa kwenye Baraza la Mawaziri.
Uteuzi huo unajiri wiki kadhaa baada ya Rais kulivunja baraza lake lote la mawaziri isipokuwa Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.
Orodha ya mwisho inajumuisha;
- Wizara ya Fedha - John Mbadi
- Wizara ya Vijana na Michezo - Kipchumba Murkomen
- Wizara ya Vyama vya Ushirika - Wycliffe Oparanya
- Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Urithi - Stellah Langa't
- Wizara ya Utalii - Rebecca Miano
- Wizara ya Nishati - Opiyo Wandayi
- Wizara ya Utumishi wa Umma - Justin Muturi
- Wizara ya Biashara - Salim Mvurya
- Wizara ya Kazi - Alfred Mutua
- Wizara ya Madini - Hassan Joho
Siku ya Ijumaa wiki jana, rais alitaja kundi la kwanza la walioteuliwa kwenye baraza lake la mawaziri akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
- Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa - Kithure Kindiki
- Wizara ya Afya - Debra Mulongo Barasa
- Wizara ya Ulinzi- Aden Duale
- Wizara ya Barabara na Uchukuzi - Davis Chirchir
- Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu - Soipan Tuya
- Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji - Eric Muga
- Wizara ya Elimu- Julius Migosi
- Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji - Alice Wahome
- Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo- Dk Andrew Karanja
- Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali- Dk Margaret Ndungu
Rais Ruto alimteua Rebecca Miano kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Miano hata hivyo amehamishwa kupelekwa wizara ya Utalii.