logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Samaki aina ya Papa katika Pwani ya Brazil wagundulika kuwa na chembechembe za Cocaine

Wote 13 walijaribiwa kuwa na dawa hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari24 July 2024 - 11:37

Muhtasari


  • • Tafiti za awali zimegundua kokeni katika maji ya mito, bahari na maji taka, na athari za dawa hiyo zimepatikana katika viumbe wengine wa baharini kama vile uduvi.
Samaki aina ya papa

Papa mwitu katika ufuo wa Brazili wamepatikana na chembechembe za cocaine, kulingana na utafiti mpya wa wanasayansi wa Brazili, katika utafiti wa hivi punde.

Kwa mujibu ripoti, utafiti huo unaonyesha jinsi matumizi haramu ya dawa za kulevya yanayofanywa na binadamu yanadhuru viumbe vya baharini.

Kulingana na utafiti wenye kichwa Cocaine Shark na kuchapishwa katika jarida la Science of the Total Environment, wanasayansi walichana miili ya papa 13 wenye ncha kali (Rhizoprionodon lalandii) walionaswa kwenye nyavu za wavuvi karibu na ufuo wa Rio de Janeiro.

Wote 13 walijaribiwa kuwa na dawa hiyo.

Tafiti za awali zimegundua kokeni katika maji ya mito, bahari na maji taka, na athari za dawa hiyo zimepatikana katika viumbe wengine wa baharini kama vile uduvi.

Utafiti tofauti hivi majuzi ulifichua kwamba viwango vya juu vya mabaki ya kokeini vilikuwa vikisababisha "athari kubwa za sumu" kwa wanyama kama vile kome wa kahawia, oysters na mikunga huko Santos Bay, katika jimbo la São Paulo la Brazili.

Lakini mkusanyiko uliopatikana katika papa wa Rio ulikuwa juu mara 100 kuliko ulivyopatikana katika wanyama wengine wa baharini, watafiti walisema.

Jinsi kokeini ilivyoishia kwenye papa bado ni kitendawili.

Kuna uwezekano kadhaa: moja ni kwamba dawa hiyo ilianguka baharini wakati wa usafirishaji au ilitupwa baharini na wasafirishaji haramu wakijaribu kukwepa mamlaka.

Brazili haizalishi kiasi kikubwa cha kokeini, lakini ni msafirishaji mkuu nje, huku magenge yenye nguvu ya mitaani kama vile First Capital Command (PCC) ikituma tani za dawa hiyo katika makontena ya usafirishaji hadi Ulaya, The Guardian waliripoti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved