logo

NOW ON AIR

Listen in Live

IGAD yajitolea kuleta amani Sudan

Vita hivi vimewaacha watu wengi bila makao huku wengi wakihamia mataifa jirani kwa minajili ya usalama.

image
na SAMUEL MAINA

Habari25 July 2024 - 12:44

Muhtasari


  • •"Wakati usaidizi wa kibinadamu umekuwa muhimu katika kupunguza mateso ya ndugu na dada zetu, amani nchini Sudan inasalia kuwa suluhisho endelevu." Alitamba Dk. Workhen Gebeyehu
  • •Washiriki walisisitiza umuhimu wa mashauriano ya mara kwa mara ili kuhakikisha uratibu na usawazishaji wa juhudi katika kusaidia mipango ya amani nchini Sudan

Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) imetoa wito wa kutatuliwa mara moja mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Akizungumza nchini Djibouti alipokutana na washirika na mashirika yanayojumuisha Ofisi mbalimbali, Wapatanishi na mipango ya Mabingwa wa Amani nchini Sudan Katibu Mtendaji wa IGAD Dk. Workhen Gebeyehu alijitolea kwa udi na uvumba katika uundaji wa Sudan yenye umoja na amani.

"Wakati usaidizi wa kibinadamu umekuwa muhimu katika kupunguza mateso ya ndugu na dada zetu, amani nchini Sudan inasalia kuwa suluhisho endelevu."

Aliwataka washirika wote wa IGAD kuungana na kushirikiana kwa juhudi na jitihada zao, kwa kuwa mbele ya uratibu ambao utakuza sauti na hatua za pamoja za kumaliza ugomvi na mizozo kama hii.

Mkutano huu unafuatia kikao cha awali cha mashauriano cha Miradi ya Amani ya Sudan kilichofanyika mapema mwezi huu katika jiji kuu la Cairo, Misri.

Washiriki walisisitiza umuhimu wa mashauriano ya mara kwa mara ili kuhakikisha uratibu na usawazishaji wa juhudi katika kusaidia mipango ya amani nchini Sudan.

Eneo la IGAD linaenea zaidi ya eneo la kilomita milioni 5.2 ambalo linajumuisha nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda.

Mkoa huu una takriban kilomita 6960 za ukanda wa pwani na Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden, Ghuba ya Toudjoura na Bahari ya Shamu.

Jukumu kuu la kimkakati la IGAD ni kukuza ushirikiano wa kikanda na ushirikiano kati ya nchi wanachama wake kwa lengo la kuboresha ustawi wa raia wote.

Ili kufanikisha hili, IGAD inafanya kazi kupitia maeneo mawili ya programu ya biashara, viwanda na utalii, na maendeleo ya miundombinu.

Vita katika taifa la Sudan vilianza mnamo 15 Aprili 2023 ambayo sasa imemaliza mwaka mmoja. Vita hivi vimewaacha watu wengi bila makao huku wengi wakihamia mataifa jirani kwa minajili ya usalama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved