logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto apendekeza Douglas Kanja kuwa IG wa polisi na kuteua manaibu wa IG

Rais pia aliwateua Eliud Kipkoech Lagat na Gilbert Masengeli manaibu wa IG.

image
na Davis Ojiambo

Habari25 July 2024 - 11:54

Muhtasari


  • • Eliud Lagat atakuwa naibu jenerali wa polisi kitengo cha polisi wa kawaida huku Gilbert Misengeli akishikilia kitengo cha polisi wa utawala (AP).

Rais William Ruto amependekeza Douglas Kanja Kirocho kuwa Inspekta Jenerali wa polisi.

Kanja amekuwa akihudumu kama kaimu Inspekta Jenerali wa polisi tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa IG Japhet Koome.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 245 (2) cha katiba Mheshimiwa Rais amemteua Bw. Douglas Kanja Kirochi kuteuliwa kuwa Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kitaifa", waraka wa rais ulisema.

Kanja ana tajiriba ya karibu miongo minne ambapo amepanda kutoka cheo cha chini hadi kufikia aliko sasa. Awali alihudumu kama naibu Jenerali wa polisi, kamanda wa kikosi cha GSU na kamanda wa polisi katika kaunti ya Kilifi.

 

Katika barua kwa tume ya Huduma kwa polisi siku ya Alhamisi Rais Ruto pia aliwateua Eliud Kipkoech Lagat na Gilbert Masengeli kuwa manaibu wa Inspekta Jenerali wa polisi.

Eliud Lagat atakuwa naibu jenerali wa polisi kitengo cha polisi wa kawaida huku Gilbert Misengeli akishikilia kitengo cha polisi wa utawala (AP).


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved