logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini DCI inataka Boniface Mwangi, wengine 4 kuzuiliwa kwa siku 21

DCI ilisema kuwa makazi ya watano hao hayajulikani na kuwaachilia kunaweza kutatiza uchunguzi.

image

Habari26 July 2024 - 11:23

Muhtasari


  • Katika ombi la DCI na kuwasilishwa kwa Mahakama ya Hakimu Mkuu Milimani, iliyoonekana na Radiojambo , wapelelezi hao wanatafuta amri ya kuzuiliwa kukamilisha uchunguzi kuhusu uhalifu uliotajwa hapo juu.
Boniface Mwangi.

Idara ya Upelelezi wa Jinai inataka kumzuilia mwanaharakati Boniface Mwangi na wengine wanne kwa siku 21 ili kuwezesha uchunguzi kukamilika.

Mwangi, Albert Wambugu, Robert Otieno, Pablo Chacha na Erot Franco wanashutumiwa kwa madai ya uchapishaji wa uwongo, kushiriki katika mkusanyiko usio halali na kuleta fujo kwa njia ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Katika ombi la DCI na kuwasilishwa kwa Mahakama ya Hakimu Mkuu Milimani, iliyoonekana na Radiojambo , wapelelezi hao wanatafuta amri ya kuzuiliwa kukamilisha uchunguzi kuhusu uhalifu uliotajwa hapo juu.

"Naomba mahakama hii tukufu itoe amri za kuwashikilia walalamikiwa katika kizuizi cha mlalamishi kwa siku 21 ili kuwezesha mlalamishi kukamilisha upelelezi wake," afisa George Karanja alisema.

Katika maombi hayo mengine ya tarehe 26 Julai, inadaiwa kuwa mnamo Alhamisi, Julai 25, 2024, mwendo wa saa 11:30 asubuhi au karibu na eneo la CBD, kando ya Mtaa wa Koinange, watano hao walisababisha uvunjifu wa amani.

DCI inadai kuwa Mwangi na wengine waliwasumbua watumiaji wengine wa barabara kwa kuziba barabara kwa kuweka jeneza jeupe na misalaba saba nyeupe iliyoandikwa majina.

DCI inadai zaidi kwamba watano hao walikuwa wakisambaza fulana na mabango yanayodaiwa kuandikwa maneno ya uchochezi.

“Kwamba wahojiwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii walichapisha madai kuwa Serikali ina lengo la kuwaua wananchi wake ambayo maneno yalichukuliwa na kutafsiriwa kuwa serikali inafanya mauaji ya kiholela; matangazo ambayo yalichochea wananchi na kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema. DCI aliambia mahakama.

Kurugenzi iliiambia Mahakama kuwa upelelezi tayari unaendelea ili kubaini nia ya kubeba vitu mbalimbali ambavyo Mwangi na wenzake walikamatwa navyo.

Zaidi ya hayo, uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali ambapo jeneza jeupe na misalaba nyeupe vilitoka na mfadhili ni nani.

DCI ilisema kuwa makazi ya watano hao hayajulikani na kuwaachilia kunaweza kutatiza uchunguzi.

Watano hao wamekamatwa na kuzuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Simu zao za rununu tayari zimechukuliwa ili kuwa chini ya uchunguzi wa cyber kwa uchambuzi.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved