logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Masengeli, Lagat Waapishwa kuwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (Picha)

DIG-APS ina jukumu la kuongoza huduma ya polisi ya utawala na inafanya kazi chini ya maelekezo na udhibiti wa IG.

image
na Davis Ojiambo

Habari26 July 2024 - 06:30

Muhtasari


  • •Jukumu la DIG-KPS linahusisha kuamuru, kudhibiti, na kusimamia huduma ya polisi ya Kenya chini ya uongozi wa IG.
  • • DIG-APS ana jukumu la kuongoza huduma ya polisi ya utawala na anafanya kazi chini ya maelekezo na udhibiti wa IG.
Jaji Mkuu Martha Koome akiwa na Eliud Lagat na Gilbert Masengeli wakati wa kuapishwa kwao katika mahakama ya juu mnamo Julai 25, 2024.

Naibu inspekta jenerali wa polisi (DIG-KPS)  Eliud Lagat na naibu inspekta jenerali wa polisi wa utawala (DIG-APS) ,Gilbert Masengeli waliapishwa Alhamisi.

Waliapishwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika mahakama ya juu na kuongozwa na Jaji mkuu na rais wa mahakama ya juu ya Kenya Martha Koome.

Inspekta Jenerali Douglas Kanja Kirocho baada ya hapo alikabidhi Kamandi ya NPS kwa Masengeli. DIG Masengeli sasa atakuwa kaimu inspekta jenerali wa jeshi la polisi nchini.

Hii inafuatia uteuzi wa Kanja kama inspekta jenerali wa polisi mnamo Juni 25, 2024, na Rais William Ruto.

Jukumu la DIG-KPS linahusisha kuamuru, kudhibiti, na kusimamia huduma ya polisi ya Kenya chini ya uongozi wa inspekta jenerali.

DIG-APS ina jukumu la kuongoza huduma ya polisi ya utawala na inafanya kazi chini ya maelekezo na udhibiti wa inspekta polisi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved