Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa akitoroka na Sakramenti takatifu katika kanisa moja la katoliki, mjini Ifakara, nchini Tanzania.
Enock George Masala alikamatwa na walinzi wa Kanisa Kuu la Mtakataifu Andrea siku ya Jumapili asubuhi baada ya kudaiwa kutekeleza uhalifu huo wa kushangaza
Inaripotiwa mshukiwa alipatikana akitoroka na sakramenti takatifu baada ya kupokea ekaristi katika kanisa hilo lililo mkoani Morogoro.
Kijana huyo alikuwa ameungana na waumini wengine wakati ya Misa ya kwanza Asubuhi ya Leo Julai 28. Wakati ibada ikiendelea, ilitangazwa Kanisani kuhusu tukio la wizi wa Sakramenti ambayo mshukiwa alitaka kutoroka nayo.
Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo la Ifakara Padre Marcus Mirwatu amesema kumekuwa na wimbi la matukio ya watu wasio wakatoliki wanaongia Kanisani kukomunika na kisha kuondoka na Sakramenti, kinyume na taratibu na miongozo ya Kanisa Hilo.
Kiongozi huyo wa Kanisa amelaani vitendo hivyo na kuaziga wakisto kuwafichua watu wenye tabia kama hiyo, ambao wanakwenda kinyume na Imani ya Kanisa hilo.
Aidha, amewataka walinzi wa Kanisa kuendelea kumuhoji kijana huyo ili kufahamu sababu za yeye kufanya kitendo hicho.
"Tunashindwa kuelewa watu hawa wanatumwa na nani kufanya vitendo hivi, hatuelewi wana malengo Gani Kwa Kanisa letu, Hivyo ninaomba kijana huyu aendelee kuhojiwa kwanini amefanya tukio Hilo" alieleza Paroko Padre Mirwatu.
Kijana huyo alipohojiwa na mwandishi wa habari alikiri kuwa yeye si Mkristo Mkatoliki, na kwamba alitenda kitendo hicho baada ya kuona Wakristo wengine wakipanga foleni na kupokea Sakramenti.
Alidai kwamba hakujua kama ni kosa kuondoka na Sakramenti Kanisani hapo huku akiweka wazi kuwa hakuna taratibu zote za kikanisa anazozijua.