KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 29.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nandi, Nyamira, Nyeri na Kirinyaga.
Katika kaunti ya Nandi, maeneo ya Chebilat na Aldai Technical yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa sita adhuhuri.
Eneo la Tombe Tea Factory katika kaunti ya Nyamira litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Skuta na Thunguma katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Thumaita na Mucagara katika kaunti ya Kirinyaga pia zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.