logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wawahoji wasaidizi watatu wa Gachagua kuhusiana na maandamano ya kupinga serikali

Polisi walizuru afisi za maafisa hao katika mtaa wa Karen, Nairobi kwa taarifa zao katika kikao kilichochukua saa nyingi.

image
na SAMUEL MAINA

Habari30 July 2024 - 12:49

Muhtasari


  • •Polisi walizuru afisi za maafisa hao katika mtaa wa Karen, Nairobi kwa taarifa zao katika kikao kilichochukua saa nyingi.
  • •Polisi wanadai watu hao walilipa wahuni waliovamia maduka na majengo mengine ili kupora wakati Gen Z wakiandamana.
DP RIGATHI GACHAGUA

Wasaidizi watatu waku wa Naibu Rais Rigathi Gachagua walihojiwa siku ya Jumanne kuhusu uchunguzi unaoendelea wa kutaka kubaini wale ambao huenda walifadhili maandamano dhidi ya serikali.

Polisi walizuru afisi za maafisa hao katika mtaa wa Karen, Nairobi kwa taarifa zao katika kikao kilichochukua saa nyingi.

Pia waliohojiwa ni wabunge wawili kutoka Nairobi.

Haya yanajiri huku maafisa wa upelelezi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai wakichunguza maandamano yenye ghasia na uporaji wa biashara jijini Nairobi na sehemu za Kati mwa Kenya.

Polisi walisema wanatarajia kurekodi taarifa kutoka kwa wanasiasa zaidi akiwemo gavana wa zamani kuhusu machafuko hayo.

Watu hao walikuwa wameitwa katika makao makuu ya DCI kwa mahojiano katika tarehe tofauti.

Polisi wanadai watu hao walilipa wahuni waliovamia maduka na majengo mengine ili kupora wakati Gen Z wakiendesha maandamano mjini.

Wamekanusha madai hayo. Wasaidizi hao ni pamoja na washauri wa mwanasiasa huyo.

Polisi wanaoshughulikia kesi hiyo walisema kuna ushahidi mdogo unaowahusisha watu hao kwa sasa.

Wanataka kupata habari zaidi kuhusu jukumu linalodaiwa watu hao walicheza katika machafuko hayo.

Timu zinazoshughulikia uchunguzi huo zimekuwa zikitegemea ujasusi, jambo ambalo walidai kuwa haliwezi kutekelezwa kwa sasa.

Kwa mfano, kumekuwa na ripoti kwamba mwanasiasa alilipa wahuni kuvamia majengo na kupora na kuwalaumu waandamanaji.

Ripoti nyingine inadokeza kuwa mwanasiasa alilipa majambazi kushambulia ofisi ya serikali na kuiteketeza.

Polisi wanaharakisha muda ili kuhakikisha kuna ushahidi iwapo upo wa kuwafungulia mashtaka washtakiwa.

Makumi ya watu walioshiriki maandamano hayo hasa Juni 25 wamefunguliwa mashtaka mbalimbali.

Uchunguzi wa kesi hizo unaendelea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved