logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Umeme kukatizwa katika kaunti 6 leo, Jumanne- KPLC

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Makueni, Trans Nzoia, Kakamega, Laikipia, na Kilifi.

image
na SAMUEL MAINA

Habari30 July 2024 - 04:34

Muhtasari


  • •KPLC imesema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Makueni, Trans Nzoia, Kakamega, Laikipia, na Kilifi.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Julai 30. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Makueni, Trans Nzoia, Kakamega, Laikipia, na Kilifi.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu kadhaa za eneo la Gikambura zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Kaumoni katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Endebes na Panacol katika kaunti ya Trans Nzoia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa saba mchana.

Katika kaunti ya Kakamega, maeneo ya Samitsi na Kalenda yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za eneo la Chasimba katika kaunti ya Kilifi pia zitakosa umeme.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Makutano na Katheri katika kaunti ya Laikipia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved