logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Umati wenye ghadhabu wateketeza gari la Sh15m lililohusika katika ajali mbaya Ruaka

Dereva wa gari hilo aina ya SUV alikimbia eneo la tukio mara baada ya ajali hiyo.

image
na SAMUEL MAINAarticle.writers[0]?.category

Habari15 October 2024 - 15:05

Muhtasari


    Watu wawili walifariki siku ya Jumatatu jioni katika ajali mbaya baada ya kugongwa na gari katika eneo la Decimo, Ruaka, eneo bunge la Kiambaa, Kaunti ya Kiambu. 

    Polisi  walisema gari aina ya Toyota Land Cruiser SUV lililohusika katika tukio hilo la kifo lilichomwa moto na kundi la watu waliokuwa na hasira kufuatia ajali hiyo.

    Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kiambaa Pius Mwanthi alisema waathiriwa, mwanaume na mwanamke, walikuwa wakijaribu kuvuka barabara kwa miguu wakati gari hilo lilipowagonga.

    Wawili hao walifariki dunia papo hapo, alisema Mwanthi na kuongeza kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

    Alizungumza juu ya kuongezeka kwa wasiwasi kwa ajali kando ya barabara katika siku za hivi majuzi.

    "Kumekuwa na ongezeko la ajali kama hizo na inatia wasiwasi. Tunaomba tahadhari kutoka kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara," alisema.

    Dereva wa gari hilo aina ya SUV alikimbia eneo la tukio mara baada ya ajali hiyo.

    Hii ni baada ya kugundua kundi la watu walikuwa wakitaka kuwaua.

    Polisi walisema tangu wakati huo wameanzisha uchunguzi kumtafuta mmiliki wa gari hilo na kubaini chanzo hasa cha ajali hiyo.

    Milli ya marehemu ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kihara kwa uchunguzi wa maiti, huku mabaki ya gari hilo yakihamishwa hadi kituo cha polisi cha Kiambaa kwa uchunguzi zaidi.

    Ajali hiyo inajiri huku kukiwa na ongezeko la visa vya ajali mbaya nchini.




    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved