logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kikao cha kumsikiliza naibu wa rais chaahirishwa kwa masaa 2 baada ya yeye kuugua

Wakili wa Gachagua ameiambia seneti kuwa mteja wake ni mgonjwa sana.

image
na Brandon Asiema

Habari17 October 2024 - 15:56

Muhtasari


  • Naibu wa rais alikuwa shahidi wa pekee kutoka upande wa utetezi kujitetea mbele ya maseneta.
  • Spika wa seneti Amason Kingi ameahirisha kikao cha kumsikiliza naibu wa rais kutokana na sababu ya naibu huyo wa rais kulazwa hospitalini.

Kikao cha kusikiliza utetezi wa naibu wa rais Rigathi Gachagua kimeairishwa hadi saa kumi na moja jioni ambapo Gachagua anatarajiwa kufika mbele ya seneti kujitetea.

Hili limetukia baada ya wakili anayewakilisha naibu huyo wa rais Paul Muite, kuambia seneti kuwa mteja wake ni mgonjwa na amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi.

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amekosa kufika mbele ya seneti kujitetea dhidi ya madai kumi na moja yaliyowasilishwa dhidi yake na bunge la kitaifa kwa bunge la seneti huku wakili wake Paul Muite akiambia seneti kuwa mteja wake ameugua..

Wakili wa Gachagua amemwomba spika Kingi kumruhusu muda wa saa mbili ili kumwona mteja wake pamoja na daktari hospitalini.

Spika Kingi kufuatia hayo amemkubalia muda huo ila amesema kwamba ikiwa naibu wa rais Rigathi Gachagua hatafika bungeni humo kwa wakati uliowekwa, maseneta wataendelea na vikao hivyo.

Kulingana na spika, suala ambalo liko mbele ya seneti linazingatia sana muda uliowekwa kukamilika


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved