logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkulima avuna malenge yenye uzani wa kilo 1128.8

Malenge iliyopewa jina Ruby ilishinda makala ya mwaka huu katika Safeway World Championship Pumpkin Weigh-Off

image
na Brandon Asiema

Habari17 October 2024 - 11:53

Muhtasari


  • Mkulima Travis Geinger alishinda katika makala ya mwaka jana kwa kuwa na malenge kubwa zaidi yenye uzani wa 2,749lbs.
  • Travis pia aliingia kwenye orodha za Guiness World Record mwaka jana kwa kuwa na malenge kubwa zaidi iliyopewa jina Michael Jordan.

Umewahi kujiuliza malenge yenye uzani mkubwa zaidi ni kilo ngapi?

Mkulima mmoja  kutoka jimbo la Minnesota nchini Marekani, ameshinda tuzo la ubingwa wa dunia Safeway World Championship Pumpkin Weigh-Off kwa kuvuna malenge yenye uzani wa 2,471lbs sawa na kilogramu 1,128.8.

Malenge hiyo iliyoitwa jina Ruby na mkulima aliyeshinda kwa jina Travis Gienger kutoka Anoka alisafiri ya mtango wa malenge hiyo hadi sehemu ya mashindano ili kushiriki katika ubingwa huo.

Ushindi wa malenge hiyo kuwa yenye uzani mkubwa Zaidi kwenye shindano la mwaka huu ilibainika baada ya kuwekwa kwenye mashine kubwa ya kupima uzani na kubainika kuwa ilikuwa na uzito wa 2,471lbs.

Gienger ameshinda katika shindano hilo kwa mara ya nne.

Travis Gienger aliingia katika kumbukumbu za Guiness World Record mwaka jana baada ya kushinda kwenye shindano hilo la Safeway World Championship Pumpkin Weigh-Off kwa kuwa na malenge yenya uzani wa 2,749lbs.

Travis ameshinda tena katika shindano la 51 la Safeway World Championship Pumpkin Weigh-Off.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved