logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rigathi Gachagua: 'Mheshimiwa Rais, Usiniue, usiue watoto wangu'

Rigathi amedai kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamejaribu kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye chakula mara mbili.

image
na BBC NEWS

Habari20 October 2024 - 15:47

Muhtasari


  •  Rigathi Gachagua, amedai kuwa, " Ruto hakuwa na nia ya kufanya kazi nami", alitaka tu kunitumia kupata watu kushinda uchaguzi", ameambia wanahabari.
  • Gachagua aliongeza kuwa alilazimika kuwatimua baadhi ya maafisa wa ujasusi katika afisi yake kwa sababu hakujihisi salama.

Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa, Rigathi Gachagua, amedai kuwa, " Ruto hakuwa na nia ya kufanya kazi nami", alitaka tu kunitumia kupata watu kushinda uchaguzi", ameambia wanahabari.

Gachagua amezungumza hayo akiwa anatoka katika Hospitali ya Karen alipokuwa anatibiwa.

Rigathi Gachagua ameendelea kudai kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamejaribu kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye chakula mara mbili.

"Kwa mara ya kwanza, niseme ilikuwa mnamo Agosti 30, huko Kisumu, walinzi wa siri waliingia chumbani kwangu Kisumu na kuingia kwa nguvu na mmoja wao akajaribu kunitilia sumu kwenye chakula changu, lakini tuligundua na tukaweza kuepuka mpango huo." Gachagua amesema.

"Nilitakiwa kuuawa kwa kuwekewa sumu, na mnamo Septemba huko Nyeri, timu nyingine ilikuja na kujaribu kunitilia sumu kwenye chakula ambacho kilichokusudiwa kuwa changu na Baraza la Wazee wa Kikuyu."

Rigathi Gachagua ameendelea kumshutumu Rais William Ruto na kudai kuwa amesaliti makubaliano waliokuwa nayo kabla ya kuingia madarakani mwaka 2022.

Gachagua aliongeza kuwa alilazimika kuwatimua baadhi ya maafisa wa ujasusi katika afisi yake kwa sababu hakujihisi salama.

Kulingana na Gachagua, aliyemwamini amemfanya akapitia kipindi kigumu mwaka mmoja uliopita.

"Kwa mwaka mmoja uliopita, imekuwa changamoto sana kwangu. Lakini mimi ni mtu mvumilivu sana, mvumilivu kweli. Kilichotokea Alhamisi kilikuwa kilele cha mateso na mfadhaiko ulioendelea kwa mwaka mmoja.

Gachagua aliendelea kudai kuwa tangu kulazwa katika hospitali ya Karen siku ya Alhamisi, watu walio karibu na rais ambao hawakutajwa wamekuwa wakipiga simu kubaini iwapo afya yake inazidi kuzorota.

"Ninasikia watu wake wengi walikuwa wakipiga simu hapa (hospitalini) wakiuliza ikiwa nimekufa, nimenusurika, kama nitapona, walikuwa wakisherehekea," Gachagua amewaambia wanahabari wakati anatoka hospitalini.


 


"Ruto atawajibika iwapo lolote litanitokea", Rigathi Gachagua amesema.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved