logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Moses Kuria awataka majaji kutomrejesha Gachagua uongozini baada ya kutimuliwa

Kuria amesema kile ambacho Mungu amekitenganisha, kusiwepo hakimu wa kukirejesha pamoja.

image
na Brandon Asiema

Habari21 October 2024 - 14:52

Muhtasari


  • Moses Kuria amewataka majaji kutotoa uamuzi wa kumrejesha Gachagua mamlakani akitumia lugha ya kimafumbo kueleza hayo.
  • Gachagua  alisema maafisa kutoka vyombo vya usalama vya siri waliingia kwenye chumba chake na kutia sumu kwenye chakula chake.

Saa chache baada ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kuhutubia wanahabari akiomba rais William Ruto asimwangamize pamoja na familia yake, mshauri mkuu wa masuala ya kiuchumi katika serikali ya Kenya Kwanza Moses Kuria, ameonekana kutoa maoni yanayolenga kumjibu Gachagua.

Kupitia ukurasa wake wa X, Moses Kuria amewataka majaji kutotoa uamuzi wa kumrejesha Gachagua mamlakani akitumia lugha ya kimafumbo kueleza hayo.

“Majaji wapendwa, mke amesema maisha yakeyako hatarini. Kwamba mume wake alijaribu kumpa umu mara mbili. Kwa nini mhatarishe maisha yake kwa kumrudisha kwenye njia ya madhara?’  Aliuliza aliyekuwa waziri Moses Kuria.

Alipokuwa akitoka hospitalini Jumapili tarehe 20, Gachagua alifichua kuwa katika ziara ya serikali kwenye kaunti ya Kisumu, maafisa kutoka vyombo vya usalama vya siri waliingia kwenye chumba chake na kutia sumu kwenye chakula chake.

Naibu rais huyo wa zamani aliongeza kusema kuwa, tukio sawia na hilo lilitukia katika kaunti ya Nyeri ambapo alikiri kwamba timu nyingine kutoka idara ya upelelezi ya taifa NIS ilijaribu kutia sumu kwenye chakula alichokuwa ameandaliwa na baraza la wazee wa Kikuyu.

Mkuu wa ushauri wa maswala ya kiuchumu amewataka majaji kufanya uamuzi wa kumwondoa Gachagua akisema kuwa kufanywa hivyo itakuwa kwa usalama wake.

Kuria aidha amesema kuwa kile ambacho Mungu amekitenganisha, kusiwepo hakimu wa kukirejesha pamoja.

Haya yote yanajiri wakati ambapo mahakama ya juu mnamo Ijumaa 18 kutoa uamuzi wa kusitishwa uapishaji wa naibu rais mteule Kithure Kindiki aliyeidhinishwa na bunge la kitaifa kwa wingi wa kura 236.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved