logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Utata huku msichana wa miaka 23 ambaye ni binti wa MCA kupatikana ameuawa Thika

Polisi wanasema mshambulizi alimdhulumu marehemu kimapenzi kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Habari21 October 2024 - 15:56

Muhtasari


  • Msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 anaripotiwa kuuawa na mwili wake kuachwa katika nyumba hiyo ya kukodi siku ya Jumatatu.
  •  MCA huyo alisema kuwa bintiye aliondoka nyumbani kwao Kamakis Jumamosi bila tatizo lolote na alionekana mwenye furaha.

Familia ya Lucy Njeri, MCA wa kuteuliwa kutoka kaunti ya Kirinyaga, inaomboleza kifo cha binti yake, Seth Nyakio Njeri ambaye mwili wake ulipatikana katika chumba cha kukodi katika eneo la Biafra mjini Thika.

 Mwanafunzi huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Zetech mwenye umri wa miaka 23 anaripotiwa kuuawa na mwili wake kuachwa katika nyumba hiyo ya kukodi siku ya Jumatatu.

 Inaripotiwa kwamba marehemu alikuwa amesafiri kutoka nyumbani kwao katika eneo la Kamakis hadi Thika kumtembelea rafiki yake na hata alikuwa amepost picha yake akiwa na marafiki zake Jumapili, Oktoba 20, kabla ya kuomba Ksh 1,000 kutoka kwa mamake, ambazo mwanasiasa huyo wa Kirinyaga alimtumia mara moja.

 Siku ya Jumatatu asubuhi, familia ilipokea simu isiyo ya kawaida kutoka kwa rafiki wa marehemu ambaye aliwajulisha kuwa Seth ameuawa.

 Familia iliarifu polisi kabla ya mwili wa msichana huyo wa miaka 23 kupatikana ukiwa uchi.

 MCA huyo alisema kuwa bintiye aliondoka nyumbani kwao Kamakis Jumamosi bila tatizo lolote na alionekana mwenye furaha.

 Wawili hao walizungumza hadi Jumapili lakini baada ya hapo juhudi za kumpata bintiye zikawa zimeambulia patupu; simu na meseji zake zilienda bila kujibiwa na jambo hilo lilimsumbua mzazi huyo.

 Shughuli za kumtafuta zilianza bila mafanikio.

 Wachunguzi sasa wanaelekeza uchunguzi wao kwa rafiki wa kiume ambaye alikasirishwa baada ya kutengana.

 Inashukiwa kuwa mwanaume huyo alipata taarifa kuhusu aliko msichana huyo, akamtongoza na kuishia kumuua.

 Wapelelezi wamerekodi taarifa kutoka kwa rafiki wa kike Seth alikuwa amemtembelea.

 Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa alikuwa amenyongwa.

 Polisi wanasema mshambulizi alimdhulumu marehemu kimapenzi kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved