Mwanaharakati Morara Kebaso ameonyesha jinsi anavyothamini uwepo wa Mungu katika maisha yake, licha ya kutumia muda mwingi katika siasa.
Kebaso, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha INJECT alidhihirisha hili baada ya kumualika padre wa kikatoliki kubariki jumba lake katika mtaa wa Kahawa Sukari.
Alichapisha video kwenye ukurasa wake wa X akionyesha jinsi Padre huyo alivyotamka Baraka na kufungua jumba hilo ambalo Kebaso alidai kupokezwa kama zawadi na mhisani mmoja.
“Tunaziona taasisi za kidini kuwa mshirika mkubwa katika harakati zetu za kuleta mabadiliko. Tuko tayari kufanya kazi na dini na madhehebu yote katika safari hii,’ aliandika kwenye video hiyo.
Kasisi huyo aliomba ulinzi na baraka kwa ajili ya nyumba ya Morara, akisema: “Tunafungua nyumba hii kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu... Tunaomba ulinzi dhidi ya mitego yote ya adui.”
Alibariki nyumba hiyo, akionyesha matumaini kwamba yeyote anayeingia atakuwa salama na kwamba makao hayo yangesimama kama ushuhuda wa imani ya Kebaso