Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la kaunti ya
Elgeyo Marakwet amehama chama hicho na kujiunga na chama tawala cha UDA.
Mwenyekiti huyo wa zamani wa ODM Micah Kigen amekaribishwa
katika chama cha rais William Ruto katika hafla iliyoongozwa na katibu mkuu wa
chama cha UDA Hassan Omar kwenye ofisi za chama hicho Hustler Plaza jijini
Nairobi.
Viongozi katika chama tawala wamemtaka Kigen kuwa balozi
mwema wa rais William Ruto mashinani baada ya kujiunga na UDA.
“Tuanataka uwe balozi
mwema wa chama cha UDA na rais William Ruto kule nyumbani.” Alisema karani wa kitaifa wa chama cha UDA.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Kigen, katibu mkuu wa UDA
Hassan Omar amemtaka Kigen kuwa mwakilishi na kutekeleza ajenda za rais William
Ruto.
“Nakukaribisha ndani ya UDA ndugu yangu Micha Kigen. Nasema kwamba ni matamanio
ya rais William Ruto sisi kuwasikiza Wakenya, kusikiliza changamoto za Wakenya
na kupaza changamoto wanazopitia wananchi.” Alisema Omar.
Kigen alikuwa amendamana na mwakilishi wa kike wa kaunti ya
Elgeyo Marakwet Carolyn Ng’elechei pamoja seneta William Kisang.
Akiwa mwandani wa Raila Odinga ndani ya chama cha Chungwa,
Kigen alijaribu kutafuta nafasi ya kuwawakilisha wakaazi wa eneo bunge la Keiyo
Kusini ila alifeli kwa kukosa kuchaguliwa.