Matokeo ya Uchaguzi

Hussein Mwinyi atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar

Tume ya uchaguzi Zanzibar yatangaza matokeo

Muhtasari

 

  • Husein Mwinyi atangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27%
  • "Nimepokea ushindi kwa mikono miwili,

 

DKT Hussein Ali Mwinyi

 

Mgombea wa chama tawala cha CCM Husein Mwinyi atangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa wa pili kwa asilimia 19.87%.

Baada ya kutangazwa mshindi Dkt.Mwinyi amesema "Nimepokea ushindi kwa mikono miwili, Nashukuru kuwa wananchi walio wengi wamenichagua mimi na chama changu cha Mapinduzi kwa miaka 5 ijayo.

Nawashukuru kwa uvumilivu na ustahamilivu ukuwa. Niwashukuru zaidi kwa kunipigia kura za kutosheleza kuwa rasi wa Zanzibar. Nitalipa Imani hii kwa utumishi uliotukuka," Dkt Mwinyi amesema.

Dkt.Mwinyi aliongeza kusema Zanzibar mpya itajengwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi , Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofuati zao.

"Mimi Hussein Mwinyi si bora kuliko CCM ushindi huu ni wa wana Wazanzibari wote ,uchaguzi sasa umekwisha turudi kujenga Zanzibar mpya.

Aidha amesisitiza wafuasi wa CCM ,washeherekee kwa ustaha bila kukwaza wengine kwa kuwa ushindi wasingepata pasipo kuwa na ushindani.