Raila Odinga apatikana na corona

Muhtasari
  • Raila Odinga apattikana na virusi vya covid-19,Madaktari wake wamethibitisha.
  • Wamesema kwamba kinara huyo anaendelea kupokea matibabu na yuko katika hali thabiti.

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amepatikana na virusi vya  corona baada ya kulazwa hospitali kwa siku mbili zilizopita.

Madaktari wake wamesema kwamba kinara huyo anaendelea kupokea matibabu na yuko katika hali thabiti.

Katika taarifa  vyombo vya habari Raila alisema kwamba licha ya kupatikana na virusi hali yake ni thabiti.

Familia yake Raila Odinga Siku ya Jumatano ilithibitisha kwamba kiongozi huyo alilazwa katika hospitali moja hapa Nairobi ingawa hali yake  ilikuwa thabiti.

 
 

Raila ambaye wiki iliyopita alikuwa na mikutano mingi ya kupigia debe mchakato wa BBI imesemekana alilazwa siku ya Jumanne baada ya kulalamika kuhusu maumivu ya mwili na uchovu.

Duru karibu na familia yake zilithibitisha kwamba Raila alipelekwa katika hospitali baada ya kuhisi maumivu.

Katika muda wa wiki mbili zilizopita kinara huyo wa ODM amekuwa na mikutano kadhaa ya kuunga mkono marekebisho ya katiba. Alikuwa amezuru kaunti za Busia na Kakamega kabla ya kuelekea pwani kwa mikutano kadhaa ya kisiasa.

Kenya siku ya Alhamisi ilirekodi visa 829 vipya vya maambukizi ya corona huku mtu mmoja akipoteza maisha yake kutokana na corona.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO