Covid-19:Wagonjwa 96 wamo ICU, Watu 750 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Wagonjwa 96 wamo ICU, Watu 750 wapatikana na corona, huku hayo yakijiri watu 2 wamepoteza maisha yao

Watu 750 wamepatikana na virusi vya Corona baada ya sampuli 6,264 kupimwa katika saa24 zilizopita na kufikisha visa hivyo kuwa 111,935.

Jumla ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,358,390,Kutoka visa hivyo 702 ni wakenya ilhali 48 ni raia wa kigeni .

Wanaume ni 411 ilhali wanawake ni 339 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 100.

Leo watu 215 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 88,209 idadi ya waliopona Corona hadi sasa.

Watu 2 wawili wamepoteza maisha yao kutokana na corona huku idadi hiyo ikifika 1,901

Kuna wagonjwa 632 waliolazwa hospitalini kote nchini huku 1,912 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .Wagonjwa 96 wapo ICU, amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.