Rais Uhuru Kenyatta amteua Martha Koome kuwa jaji mkuu

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amteua Martha Koome kuwa jaji mkuu
Jaji Martha Koome
Jaji Martha Koome
Image: HISANI

Rais Uhuru Kenyatta siku ya JUmatano alimteua Martha Koome kuwa jaji mkuu hii ni baada ya bunge kumuidhinisha pia siku ya Jumatano.

Koome alichunguzwa na Kamati ya Haki na Maswala ya Sheria Alhamisi iliyopita, na alipewa hati safi katika harakati zake za kumrithi Jaji David Maraga, ambaye alistaafu Desemba iliyopita.

Spika Justin Muturi aliitisha kikao kupitia arifa ya Gazeti rasmi la serikali siku ya Jumatatu.

Wabunge walifanya kikao asubuhi na kingine mchana.

Wakati wa uhakiki wake, Koome aliahidi kurejesha maelewano na kumaliza uhasama kati ya Mahakama na Bunge.

Koome atachukua wadhifa wake David Maraga.

Koome alikuwa ameonya maafisa wafisadi katika Mahakama kwamba atatoa mifano ya kuonya wengine.

Jaji huyo wa mahakama ya rufaa alitoa maoni hayo wakati akihakikiwa na Kamati ya bunge ya haki na sheria.