Seneta mteule Victor Prengei ameaga dunia

Muhtasari
  • Habari hiyo ilithibitishwa na spika wa Seneti Kenneth Lusaka
  • Prengei alikuwa seneta aliyeteuliwa na Jubilee
Image: Hisani

Seneta mteule Victor Prengei ameaga dunia,Prengei alikufa katika ajali ya barabara ya Kabarak-Nakuru Jumatatu usiku.

Habari hiyo ilithibitishwa na spika wa Seneti Kenneth Lusaka.

Prengei alikuwa seneta aliyeteuliwa na Jubilee.

Alikuwa miongoni mwa maseneta sita waliokabiliwa na kamati ya nidhamu ya Jubilee mapema mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru Beatrice Kiraguri alisema kuwa Seneta huyo alikuwa akielekea eneo la Kabarak kutoka mji wa Nakuru wakati alihusika katika ajali ya gari katika eneo la Gioto.

Alifariki katika Hospitali ya Nakuru Level Five ambapo alikuwa amekimbizwa kwa matibabu.

Millicent Omanga alituma risala za Rambi rambi, kwa familia huku akisema kwamba Victor alikuwa rafiki wa kutunzwa.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.