Rais Uhuru Kenyatta ameongeza hatua za kuzuia Covid-19 kwa siku 60

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta ameongeza hatua za kuzuia Covid-19 kwa siku nyingine 60

Rais Uhuru Kenyatta aongeza hatua za kuzuia Covid-19 kwa siku nyingine 60 baada ya mkutano na viongozi wa upinzani ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Rais Uhuru Kenyatta ameongeza hatua za kuzuia Covid-19 kwa siku nyingine 60.

Hii ilikuwa baada ya mkutano na viongozi wa upinzani ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Jumatano.

Hatua hizo zinalenga kuzuia kuenea kwa janga la Covid-19 ambalo kufikia Jumatano jumla ya watu waliopatikana na corona ilifika 224,400.

Hatua za kuzuia ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne hadi saa kumi alfajiri.

Mikusanyiko na mikutano ya hadhara ya  watu, pamoja na mikutano ya kisiasa na mikutano ya kampeni ya uchaguzi unaokaribia pia imemamishwa kwa siku 60 zaidi.