ICJ yakataa kesi ya Kenya katika mzozo wa mpaka wa baharini na Somalia

Muhtasari
  • ICJ yakataa kesi ya Kenya katika mzozo wa mpaka wa baharini na Somalia

Mahakama ya UN imeamua kwa kiasi kikubwa kuipendelea Somalia katika mzozo wake wa muda mrefu na Kenya juu ya mpaka wao wa baharini.

Kenya hapo awali ilishutumu Korti ya Haki ya Kimataifa kwa upendeleo na ikasema haitakubali uamuzi huo.

Kesi hiyo ilihusu pembetatu ya kilomita za mraba 38,000 katika Bahari ya Hindi ambayo inadhaniwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi.

Mzozo huo umekuwa kiini cha mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo majirani.

Kwa miongo minne iliyopita, Kenya imesema mstari unaoeleka mashariki mwa mahali ambapo nchi hizo mbili zinakutana pwani zinawakilisha mpaka wa baharini.

Somalia, hata hivyo, ilisema kortini kwamba mpaka wa bahari unapaswa kufuata mwelekeo sawa na mpaka wa ardhi.

Jopo la majaji 14 waliokaa The Hague lilisema kwamba Kenya haijathibitisha kuwa Somalia hapo awali ilikubaliana na mpaka wake uliodaiwa.

Badala yake, walichora laini mpya ambayo imegawanya eneo lenye mgogoro mara mbili.

Lakini huku Kenya ikikataa kutambua mamlaka ya ICJ sasa haijulikani ni nini kitatokea. Korti haina njia ya kutekeleza maamuzi yake.

Mnamo 2009, nchi hizo mbili zilikubaliana katika hati ya makubaliano, ikiungwa mkono na UN, kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.

Lakini miaka mitano baadaye, Somalia ilisema mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda kwa ICJ. Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Somalia ilikasirishwa na Kenya kuuza leseni za uchunguzi wa raslimali za mafuta na gesi katika eneo lenye mzozo kwa mataifa mawili mnamo 2012.

Image: ICJ

Akiongea kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, Naibu Waziri Mkuu wa Somalia Mahdi Mohamed Guled aliambia BBC kwamba nchi yake "inaamini katika mfumo wa sheria ... ndio sababu tukafika kortini".

Korti inapaswa kuwa mwamuzi wa mwisho katika mizozo kati ya mataifa.

Kenya ilijaribu kuzuia bila mafanikio kwamba ICJ haifai kuhusika kwani hati ya makubaliano ilifaa kuzingatiwa .

Halafu mnamo Machi ilikataa kushiriki katika vikao baada ya kuuliza kucheleweshwa kwa vikao ili kuweza kutoa taarifa kwa timu mpya ya mawakili wake

Pia ilipinga uwepo katika jopo la majaji wa ICJ jaji wa Somalia, ikisema anapaswa kujiondoa.

Wiki iliyopita, serikali ya Kenya ilielezea kesi hiyo kama "mchakato wa mahakama wenye makosa". Iliongeza kuwa kulikuwa na "upendeleo wa asili" na kwamba korti hiyo ilikuwa njia isiyofaa ya kutatua mzozo huo.