Mshukiwa aliyekiri kuwauwa watoto atoweka kutoka kituo cha polisi cha jogoo

Muhtasari
  • Mshukiwa aliyekiri kuwauawa watoto atoweka kutoka kituo cha polisi cha jogoo
Mshukiwa Masten Milimu Wanjala
Image: DCI

Jamaa aliyekamatwa mapema mwezi wa Julai na kukiri kuteka nyara na kuua watoto wawili kinyama kisha kutupa miili yao maeneo ya Kabete na kuhusika kwenye mauaji zaidi ya kumi ametoweka.

Wapelelezi wa DCI walibaini kuwa Masten Milimu Wanjala, 20, ameua kinyama angalau watoto wengine kumi ndani ya kipindi cha miaka tano ambayo imepita.

Kulingana na maafisa wa DCI, Wanjala alitekeleza mauaji hayo bila huruma kwa wakati mwingine akinyonya damu kutoka kwa mishipa ya watoto hao kabla ya kuwaua.

Masten Wanjala amekimbia kutoka kituo cha polisi cha Jogoo katika hali isiyojulikana.

Polisi wanasema alikuwa anatarajiwa mahakamani leo na kwamba kusakwa kwake kunaendelea.

Muuaji wa 'Vampire' aliyekiri alifungwa kwa siku 30 ili polisi kuchunguza zaidi  mauaji ya watoto nane.

Polisi walisema idadi ya waathirika huenda ikawa ni 13, karibu wavulana wote.

Wanjala alikuwa  mbele ya hakimu mkuu wa Makadara Angello Kithinji wakati polisi walisema walihitaji muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi.