Ann Kananu amteuwa Paul Mutunga kuwa naibu gavana

Muhtasari
  • Ann Kananu amteuwa Paul Mutunga kuwa naibu gavana 
Paul Mutunga
Image: Hisani

Gavana mpya wa Nairobi Ann Kananu aliyeapishwa hivi karibuni alimteua aliyekuwa diwani Paul Mutunga Mutungi kuwa naibu wake.

Katika taarifa yake mnamo Jumatano, Novemba 17, Kananu alielezea nia yake ya kutaka kuwa naibu wake Mutungi ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi katika Ikulu ya Jiji.

Mutungi aliteuliwa kama Mkuu wa Majeshi na aliyekuwa kaimu Gavana wa Nairobi na Spika wa sasa Benson Mutura kuchukua nafasi ya Brian Kamau Mugo Januari 2021.

Uteuzi huo utawasilishwa mbele ya Bunge la Kaunti ya Nairobi ambapo wawakilishi wadi  wataidhinisha au kuukataa kupitia kwa kupiga kura.

Iwapo atafaulu, Mutungi atakuwa Naibu Gavana wa Nairobi wa nne.