Bwenyenye Jimi Wanjigi atiwa mbaroni, baada ya kuzingirwa kwa saa 20

Muhtasari
  • Bwenyenye Jimi Wanjigi atiwa mbaroni, baada ya kuzingirwa kwa saa 20
JImi Wanjigi akiwa kwenye kituo cha polisi cha Kamukunji Januari 18/2022
Image: Andrew Kasuku

MfanyIbiashara Jimi Wanjigi amekamatwa kutoka  kwa nyumba yake baada ya kuzingirwa kwa saa 20.

Allitolewa kwenye uwanja wake baada ya  polisi kuvunja ndani ya nyumba yake.

Wanjigi yuko njiani kwenda katika kituo cha polisi cha Kamkunji kwa ajili ya kuhojiwa.

Mgombea urais huyo alisema tukio hilo lilikuwa limefungwa kwa kisiasa kutokana na msimamo wake wa kisiasa na zaidi, maneno aliyofanya mwishoni mwa wiki.

Image: Andrew Kasuku

Mapema siku ya JUmanne polisi waliwatawanya viajana ambao walikuwa wamekita kambi, kwa kuandamana katika afisi za Wanjigi.

Wengine walikuwa wamekuja ndani ya mabasi matatu na kabla ya kushindwa, polisi walilazimika kutupa vitoa machozi kulazimisha madereva kuharakisha.

Kukamatwa kwake Wanjigi kuna jiri saa chache baada ya mahakama kutoa ilani ya kukamatwa kwake.