logo

NOW ON AIR

Listen in Live

UDA chawapokea MCAs 40 kutoka Meru na Tharaka Nithi

Ruto amewapokea MCAs 40 kutoka kaunti za Meru na Tharaka Nithi.

image
na Davis Ojiambo

Habari14 March 2022 - 11:37

Muhtasari


  • • Chama ch UDA kimewapokea wajumbe wa kaunti zaidi ya 40 kutoka kaunti za Meru na Tharaka Nithi, siku mbili tu baada ya kuwapokea wengine 30 kutoka Kiambu.
Ruto akiwapokea MCAs katika makazi yake, Karen

Naibu rais William Ruto amewapokea wajumbe wa bunge la kaunti zaidi ya 40 kutoka kaunti za Meru na Tharaka Nithi.

Wajumbe hao wote wanasemekana kukiasi chama tawala cha Jubilee na kujiunga na kile cha naibu rais cha UDA kama njia moja ya kujihakikishia nafasi nzuri kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Hatua hii inakuja siku mbili tu baada na naibu rais kuwapokea katika chama cha UDA tena wajumbe wa kaunti ya Kiambu zaidi ya 30 waliochaguliwa kwa kupigiwa kura kupitia chama tawala cha Jubilee ambacho kinaendelea kutorokwa na wengi huku wakionekana kuwa na upendeleo mkubwa kwa chama kipya kabisa cha UDA.

Ruto anatarajiwa kutangazwa rasmi kesho kama mgombea urais wa chama hicho baada ya kamati ya uchaguzi ya chama ch UDA kumpitisha bila kupingwa wikendi iliyopita.

Atamenyana na mwenzake kutoka muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga katika uchaguzi wa Agosti 9.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved