"Kibaki alikuwa mcheshi, kama baba wa taifa" Kalonzo, Raila wamuomboleza Kibaki

Muhtasari

• Kinara wa ODM na Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka wamemuomboleza Mwaki Kibaki kama rafiki na baba wa taifa.

Rais wa 3 wa Kenya, Mwai Kibaki
Rais wa 3 wa Kenya, Mwai Kibaki
Image: Twitter

Aliyekuwa makamu wa rais Mwai Kibaki Kalonzo Musyoka pia hachaachwa nyuma katika kuungana na taifa kwa ujumla ili kuuomboleza hayati rais wa tatu Mwai Kibaki ambaye kifo chake kilitangazwa mapema Ijumaa na rais Uhuru Kenyatta.

Kalonzo amemuomboleza Kibaki kama shina la taifa aliyechukua picha kama baba wa taifa. Kalonzo alisema kwamba Kibaki alikuwa mcheshi ambaye matamshi yake ya kuchekesha yaliwavunja mbaavu wakenya wengi kwa kutumia maneno ambayo vijana wadogo hawakukubaliwa kuyatumia hadharani.

Kinara wa Azimio-One Kenya Raila Odinga amemuomboleza hayati rais Mwai Kibaki kama Rafiki wa karibu ambaye walishirikiana vizuri katika serikali ya nusu mkate ya mwaka 2008-2012.

Akizungumza kutoka ukumbi wa KICC jijini Nairobi mapema Ijumaa, Raila alimuomboleza Kibaki kaam mtu aliyefanya kazi katika uongozi wake kuanzia mwaka 2002 aliposema Kibaki tosha, baadae akawa hasimu wake wa kisiasa kama kiongozi wa upinzani na hatimaye wakafanya kazi pamoja Kibaki akiwa rais huku Raila akiwa Waziri mkuu.