Kibaki alipenda amani, alituma KDF Somali kuwaondoa Al Shabaab - Wetangula

Muhtasari

• Moses Wetangula amemuomboleza rais Kibaki kama mtu aliyependa amani, na kusaidia kutuma KDF Somali kudhibiti Al Shabaab.

Rais mstaafu Mwai KIbaki
Image: state house

Kiongozi wa chama cha FORD-K Moses Wetangula ambaye pia ni mmoja wa vinara wa muungano wa Kenya Kwanza amemuomboleza aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya hayati Mwai Kibaki.

Akizungumza katika runinga moja humu nchini pindi tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangaza habari hizo za tanzia, Wetangula alimuomboleza rais Kibaki kama kiongozi aliyefanya kazi yake kwa umahiri mkubwa na kuimarisha uchumi ambao wakenya wanaufurahikia leo hii.

Alimuomboleza Kibaki kuwa rais aliyependa amani na kutuma majeshi ya Kenya nchini Somali chini ya mkataba wa Amison ili kulisaidia taifa hilo kupata udhibiti wa kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Kando na Somali, Wetangula pia alisema Kibaki alisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujaribu kudhibiti mgogoro wa mara kwa mara katika taifa hilo lenye utajiri wa madini.

Buriani Kibaki.