Matiang'i - Kibaki hakuwa anastahimili mambo madogo madogo ya kisiasa

Muhtasari

• Matiang'i“ - Kutostahimili kwake mambo madogo madogo ya kisiasa na maonyesho ya kando yanayopendelea vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa kutasalia kama kumbukumbu"

Fred Matiang'i na Mwai Kibaki
Fred Matiang'i na Mwai Kibaki
Image: Twitter

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i pia hajasazwa katika kutoa risala za rambirambi kwa kifo cha aliyekuwa rais wa tatu Mwai Kibaki.

Matiang’i amemuomboleza Kibaki kama mtu ambaye alikuwa na misimamo mikali, mtu asiyetetereka na woga wowote.

Alisema kiongozi huyo alikuwa ni mtu asiye na mazoea ya kustahimili mambo fulani ambayo yalikuwqa yanapindisha kinyume na ukawaida na pia mtu aliyetoa kipaumbele katika maendeleo ya miundo msingi na uchumi pia.

“Kutostahimili kwake mambo madogo madogo ya kisiasa na maonyesho ya kando yanayopendelea vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa kutasalia kuwa urithi ulioimarishwa wa kusifiwa na kuigwa,” ameandika Matiang’i kupitia Twitter yake.