Hayati Mwai Kibaki kuzikwa Jumamosi wiki ijayo

Muhtasari

•Mwili wa Kibaki utawekwa katika bunge la kitaifa kwa siku tatu kati ya Jumatatu na Jumatano ili kupatia Wakenya fursa ya kuona mwili na kutoa heshima za mwisho kwa hayati.

Hayati Mwai Kibaki ambaye alifariki Aprili 22, 2022
Hayati Mwai Kibaki ambaye alifariki Aprili 22, 2022
Image: MAKTABA

Mwili wa hayati  Emillio Mwai Kibaki utazikwa siku ya Jumamosi, Aprili 30 nyumbani kwake Othoya, kaunti ya Nyeri.

Waziri wa masuala ya ndani Fred Matiang'i ametangaza kwamba kamati ya kuandaa mazishi ya hayati imekamilisha mipango yake.

Akuzungumza katika Harambee House Jumamosi, Matiang'i alisema mwili wa Kibaki utawekwa katika bunge la kitaifa kwa siku tatu kati ya Jumatatu na Jumatano ili kupatia Wakenya fursa ya kuona mwili na kutoa heshima za mwisho kwa hayati.

"Kutakuwa na mazishi ya kitaifa ya hayati Mwai Kibaki.Ningependa umma ufahamu kwamba hafla hiyo itafanyika Ijumaa, Aprili  29, 2022 katika uwanja wa Nyayo. Rais Kibaki atazikwa huko  Othaya, Nyeri siku ya Jumamosi Aprili 30, 2022," Matiang'i alisema.

Kifo cha Kibaki kilitangazwa siku ya Ijumaa, Aprili 22.  Hayati alifariki akiwa na umri wa miaka 90.