Matiang'i atangaza Jumanne sikukuu ya umma kusherehekea Idd

Muhtasari
  • Matiang'i atangaza Jumanne sikukuu ya umma kusherehekea Idd
Waziri wa usalama Fred Matiang'i
Image: FRED MATIANG'I/TWITTER

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi ametangaza Jumanne kuwa sikukuu ya kusherehekea Idd-ul-Fitr.

Katika notisi ya gazeti la serikali mnamo Jumanne, Matiang'i alitangaza Mei 3 kuwa sikukuu ya umma kwa kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Likizo ya Umma.

Sikukuu ya Idd-ul-Fitr, Sikukuu ya Kufungua Mfungo, ni sikukuu muhimu ya kidini inayoadhimishwa na Waislamu ulimwenguni kote ambayo inaadhimisha mwisho wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa Kiislamu wa mfungo.

Waislamu husherehekea Idd-ul-Fitr kwa sala zinazoitwa "Salat Al Eid" kwa Kiarabu.