4 wauawa baada ya maafisa GSU kufyatulia risasi kundi la kinamama eneo barabara kuu ya Mombasa

Muhtasari

• Kundi hilo la wanawake lilikuwa linaandamana kuonyesha hasira zao kufuatia kifo cha mwalimu aliyeripotiwa kuuawa na tembo. 

crime scene
crime scene

Maafisa wa GSU wamewaua watu wanne papo hapo baada ya kuwafyatulia risasi huko Kajiado. 

Maafisa hao walikuwa wakijaribu kuwatawanya wanawake waandamanaji katika eneo la Masimba walipowafyatulia risasi na kuua wanne na kujeruhi wengine saba. 

Maandamano hayo yalikuwa yameandaliwa na kundi la wanawake wanaotaka kuchukuliwa hatua kwa mgogoro baina ya binadamu na wanyamapori. 

Kundi hilo la wanawake lilikuwa linaandamana kuonyesha hasira zao kufuatia kifo cha mwalimu aliyeripotiwa kuuawa na tembo. 

Walikuwa wakielekea kwa afisi za shirika la Wanyamapori KWS na kisha wakafunga barabara kuu ya Nairobi-Mombasa. 

Katika vurumai zilizofuata, maafisa wa GSU waliokuwa wakielekea Mombasa kwa lori walijaribu kuingilia kati na kutuliza hali lakini mambo yalienda mrama na kupelekea maafisa hao kuwafyatulia risasi.