Mwaniaji wa ODM katika wadi ya South Gem Nick Wanga amefariki

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 anasemekana kufariki kutokana na malaria ya ubongo kulingana na kaka yake.

Muhtasari
  • Kulingana na msemaji wa familia Abala Wanga, marehemu mwanasiasa, Nick Wanga alifariki Jumamosi mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi katika hospitali ya Agha Khan mjini Kisumu
NICK WANGA
Image: ODM/TWITTER

Chama cha Orange Party mapema Jumamosi kilipoteza mgombeaji wa wadi ya South Gem.

Kulingana na msemaji wa familia Abala Wanga, marehemu mwanasiasa, Nick Wanga alifariki Jumamosi mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi katika hospitali ya Agha Khan mjini Kisumu.

Abala ambaye ni meneja wa Jiji la Kisumu alisema mdogo wake alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo alikolazwa siku tatu zilizopita.

"Ni siku ya huzuni kwetu kama familia kumpoteza kijana ambaye alikuwa na mustakabali mzuri mbele yake," alisema.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 anasemekana kufariki kutokana na malaria ya ubongo kulingana na kaka yake.

"Alikuwa sawa. Alikuwa miongoni mwa timu iliyokutana na Jalang'o Midiwo nyumbani kwake ili kujadili njia ya kuendeleza siasa za eneo bunge la Gem," alisema.

Jumapili iliyopita, marehemu Wanga alikutana na sekretarieti yake ya kampeni ili kuweka mikakati ya jinsi ya kunyakua kiti cha wadi ya South Gem.

Msemaji wa familia alisema maandalizi ya mazishi yatawasilishwa baadaye.

Chama cha ODM kikituma risala za rambirambi kilisema kwamba kimehuzunishwa na kifo chake Nick, huku uchaguzi ukiawa umesalia siku 30 pekee.

"Tumehuzunishwa na kifo cha Mhe. Nick Wanga, mgombea wetu wa kiti cha Wadi ya Gem Kusini katika Gem Const ya Kaunti ya Siaya mapema leo. Inasikitisha kwamba Nick amepitisha siku 32 kwenye Uchaguzi Mkuu. Tunaomba kwa ajili ya familia na watu wa South Gem wakati huu wa majaribu."