BACK TO SCHOOL

Njia tano za wazazi kuokoa pesa kwenye vifaa vya kurudi shuleni

Je, ni mbinu gani umetumia ili kuhakikisha kwamba haufilisiki wakati unapofanya ununuzi wa back to school?

Muhtasari
  • Maduka ya Naivas daima yanajaribu kutafuta njia za kuhakikisha yanasawazisha bei kwa ajili yako. Maduka hayo yako tayari sana, haswa kwa mahitaji yako ya msimu huu wa Back to school.
  • Hapa kuna vidokezo vichache ambavyo wazazi hutumia kuokoa pesa halisi

Ni msimu mwingine wa wanafunzi kurejea shuleni almaarufu ‘back to school’, ambacho ni kipindi chenye msongo wa mawazo kwa wazazi wengi kutokana na nyakati ngumu za kiuchumi na gharama ya maisha inayoongezeka kila mara.

Kuanzia kununua nguo mpya, usafiri, vifaa vya shule na vyakula mbalimbali, mara nyingi huonekana kuwa nyingi kwa wakati mmoja.

Je, ni mbinu gani umetumia ili kuhakikisha kwamba haufilisiki wakati unapofanya ununuzi huo?

Maryanne Kadzo, fundi wa nguo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Kangemi, anasema anapofanya manunuzi ya kurudi shuleni, anahakikisha anawanunulia watoto wake wawili bidhaa kwa wingi ili kuokoa baadhi ya sarafu.

"Pia namsisitizia mzaliwa wangu wa kwanza kutunza sana sare zake, vitabu, viatu ili kumkabidhi dadake mdogo kwani hii inaniokoa pesa," Kadzo anasema.Kuna njia nyingi za kuokoa pesa kwenye mahitaji yako ya Back to school.

Hapa kuna vidokezo vichache ambavyo wazazi hutumia kuokoa pesa halisi

1. Kununua vifaa vya shule kwa wingi ili kuokoa pesa - Baadhi ya bidhaa ni nafuu zinaponunuliwa kwa jumla kama vile kununua pakiti ya kalamu badala ya moja tu, na hivyo una ugavi wa kutumika kwa mwaka mzima shuleni.

2. Pata manufaa ya mapunguzo ya bei ya bidhaa, kwa kimombo discount - Linganisha bei katika maduka mbalimbali ili kuhakikisha kuwa unanunua bidhaa zenye ofa bora zaidi.

3. Nunua tu unachohitaji - Kabla hata hujaanza kufanya ununuzi, tembea kwenye vyumba vyote nyumbani mwako ili kuorodhesha kile ambacho tayari unacho. Sio lazima kununua nguo nyingi na vifaa vipya vya shule ambavyo hawatahitaji.

4. Fuata orodha ya ununuzi/bajeti iliyoundwa - Njia bora ya kuokoa hela zako kwenye ununuzi wa Back to school ni kutengeneza bajeti kabla hata ya msimu huo. Kisha, jitahidi sana kuzingatia bajeti hii. Mojawapo ya njia rahisi zaidi za kutumia pesa nyingi ni kufanya ununuzi bila vikwazo vya kifedha.

5. Fuata maduka kama vile duka la jumla la Naivas kwenye mitandao ya kijamii na uwashe arifa za machapisho, ama ‘post notification’. Kwa njia hiyo, wanapoanza kutuma mauzo na ofa kwa ajili ya ununuzi wa kurudi shuleni, utaarifiwa ili usikose.



Maduka ya Naivas daima yanajaribu kutafuta njia za kuhakikisha yanasawazisha bei kwa ajili yako. Maduka hayo yako tayari sana, haswa kwa mahitaji yako ya msimu huu wa Back to school.

Unaweza kuingia katika mojawapo ya maduka 84 ya Naivas na kufurahia manufaa yanayoletwa na kununua bidhaa zako Naivas. Hii ikijumuisha duka lao mpya la NaivasFoodmarket pale Safari Center katika eneo la Kayole, kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Unaweza kununua na kufurahia bei bora zaidi ya kila siku kwenye maduka yote ya Naivas kwa, mahitaji yako ya Kurudi Shuleni. Wana matoleo bora zaidi ya mauzo (discounts) kwa bidhaa za aina zote.Rudi Shuleni kwa njia halisi ya Kikenya na Naivas Back To School.

Naivas...saves you money!