Shule zote kufunguliwa Agosti 15 - Waziri Magoha

Magoha alitoa tangazo la kufungwa kwa shule ili kuipa IEBC nafasi ya kujiweka tayari kwqa uchaguzi.

Muhtasari

• Shule zote zilifungwa wiki jana katika tangazo la ghafla kutoka kwa waziri Magoha aliyetaka shule kufungwa.

• Wazazi walilipokea tangazo hilo kwa mshangao mkubwa na kumfokea vikali Magoha ambaye siku chache baadae aliomba radhi ya kutoa tangazo ghafla.

Waziri wa Elimu George Magoha akihutubia wanahabari Kisumu mnamo Machi 21, 2022.
Waziri wa Elimu George Magoha akihutubia wanahabari Kisumu mnamo Machi 21, 2022.
Image: FAITH MATETE

Waziri wa elimu msomi George Magoha ametangaza kwamab shule zitafunguliwa kote nchini mnamo tarehe 15 Agosti, siku kadhaa baada ya kufungwa kwa ajili ya kutoa nafasi ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutumia baadhi ya shule kama vituo vya kupiga kura.

Magoha aliwashtua wazazi na washika dau wengi katika sekta ya elimu kwa kutoa tangazo la ghafla kutaka shule zote nchini Kenya kufungwa mara moja, jambo ambalo lilisambaratisha shughuli nyingi katika taasisi za kusoma.

Magoha alisema wizara imefahamishwa kuwa huenda mchakato wa kujumlisha kura bado unaendelea katika tarehe iliyotajwa.

“Kwa hiyo, kufuatia mashauriano zaidi, nawasilisha uamuzi wa Serikali kwamba Vyuo vya Elimu ya Msingi vitafunguliwa kuanzia Jumatatu, tarehe 15 Agosti 2022,” alisema Waziri Magoha.

Awqali, agizo la ghafla la kufunguwa kwa shule lilizua mdahalo mkubwa nchini huku wazazi wengi wakilalamikia hali ya kutojali kwa upande wa wizara ya elimu.

Mdahalo huu ulimfanya waziri akaomba radhi wazi wazi kwa wazazi na washikadau wote katika sekta ya elimu.

"Baada ya mashauriano, nawasilisha uamuzi wa Serikali kuhusu kufungwa mara moja kwa vyuo vyote vya elimu ya msingi kuanzia Jumanne, Agosti 2 hadi Jumatano, Agosti 10 ili kuhakikisha kuwa maandalizi na uendeshaji wa chaguzi zijazo unafanyika bila matatizo," CS Magoha alisema katika taarifa yake siku ya Jumatatu.  

"Tunaomba radhi kwa mkanganyiko uliotokea kutokana na mabadiliko haya ya tarehe na tunawauliza wote kushirikiana na sisi katika kufanya kazi kuhakikisha usalama na utulivu wa watoto wetu katika taasisi za masomo, tangazo hili linabatilisha tangazo la awali lililotaka shule kufunguliwa Agosti 11," Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisoma.