Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa hatimaye Amejisalimisha kwa Polisi

Barasa alitetea kiti chake kupitia tikiti ya UDA

Muhtasari

• Jana, DCI ilikuwa imempa makataa ya saa sita kujisalimisha la sivyo msako mkali dhidi yake uanzishwe mara moja.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa
Image: MAKTABA

Mbunge wa Kimilili kupitia chama cha UDA, Didmus Barasa hatimaye amejisalimisha kwa vyombo vya usalama, siku moja tu baada ya kitengo cha upelelezi wa jinai DCI kutangaza msako dhidi yake kwa tuhuma za mauaji ya mlinzi wa mshindani wake wa kisiasa, Brian Kahemba.

Alhamis, DCI ilitoa taarifa kwa umma kwamba ilikuwa imempa Barasa chini ya saa sita tu kujisalimisha kwenye mikono salama ya kisheria la sivyo msako mkali dhidi yake ungeanzishwa na kumtia mbaroni.

"Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai inamuonya Mhe Didmus Barasa, ambaye amejificha baada ya mauaji ya kikatili ya Brian Olunga, kujisalimisha kwa kituo cha polisi kilicho karibu ndani ya saa 6 zijazo. Mhe Barasa, anasakwa kwa mauaji ya Brian, ambaye alimpiga risasi paji la uso na kumuua papo hapo, mnamo Jumanne, Agosti 8, eneo la Chebukwabi huko Kimilili, kaunti ya Bungoma," sehemu ya ripoti hiyo ya DCI ilisema.

Barasa ambaye alitangazwa kushinda wadhfa wa ubunge kimilili kwa mara ya pili alisemekana kutorokea kusikojulikana mnamo Jumanne usiku baada ya kumpiga risasi mlinzi wa mshindani wake ambaye walizozana katika kituo kimoja cha kupigia kura.

Barasa alijisalimisha baada ya idara ya DCI siku ya Alhamisi kutoa makataa ya saa sita kujisalimisha.

Alikuwa ametakiwa kujisalisha kwa kituo cha polisi kilicho karibu naye.

Baraza anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Brian Olunga, msaidizi wa mpinzani wake wa kisiasa.

Ikiwa hangejisalimisha, DCI walikuwa waanzishe msako kumtia mbaroni, alikuwa meenda mafichoni kwa siku tatu.

"Kikosi maalumu cha maafisa wa ujasusi kutoka kitengo cha  Utafiti wa Uhalifu na Mauaji kimetumwa ili kuimarisha zoezi la kumtafuta."

Barasa anadaiwa kumpiga risasi Olunga katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi usiku wa Agosti 9.

Barasa inasemekama alitoa bastola na kumlenga Brian Olunga na kumpiga risasi usoni ambapo alivuja damu nyingi.

Barasa alitetea kiti chake kupitia tikiti ya UDA  ila baada ya kutangazwa, ajenti wake alinyimwa cheti chake huku msimamizi wa uchaguzi katika kaunti hiyo alikataa ombi hilo la wakala wake na kumtaka Barasa mwenyewe kujisalimisha na kukabidhiwa cheti hicho cha ushindi.