Mahakama ya upeo imedumisha ushindi wa Ruto kama rais wa 5 wa Kenya

Hii ni baada ya mahakama ya upeo kudumisha ushindi wake adhuhuri ya Jumatatu.

Muhtasari

• Majaji wa mahakama ya upeo ni Jaji mkuu Martha Koome, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu, Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u, Isaac Lenaola, William Ouko na Mohamed Ibrahim.

Rais wa tano wa Kenya
WILLIAM RUTO Rais wa tano wa Kenya
Image: Facebook//WILLIAMRUTO

Ni rasmi sasa kwamba William Ruto  atakuwa rais wa tano wa Kenya.

Hii ni baada ya Jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo likiongozwa na jaji mkuu Martha Koome kuidhinisha ushindi wa rais mteule William Ruto.

Jopo hilo likisoma uamuzi wake lilisema kwamba kesi iliyowasilishwa katika mahakama hiyo na muungano wa Azimio la Umoja pamoja na mashirika mengine haikudhihirisha wazi malalamisho yao haikuwa na uzito unaoweza kufanya ushindi wa Ruto kubatilishwa.

Kando na jaji mkuu Martha Koome, majaji wengine walikuwa ni pamoja na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu, Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u, Isaac Lenaola, William Ouko na Mohamed Ibrahim.

Mahakama hiyo ilitupilia mbali madai yote yalioibuliwa na waliopinga ushindi wa Ruto na ikiwemo kuafikia kigezo cha sheria kuwa mshindi wa urais anafaa kufikisha asilimia 50+1.