Meru:Gavana Mwangaza abanduliwa mamlakani

Wabunge wa Bunge la Kaunti ya Meru waliwasilisha hoja ya kumtimua gavana huyo Jumatano asubuhi.

Muhtasari
  • Hoja ya kumshtaki ilikamilika baada ya MCAs kuunga mkono kwa kiasi kikubwa
(KUSHOTO) MUMEWE GAVANA WA MERU MUREGA BAICU.(KATI)GAVANA MWANGAZA KAWIRA,(KULIA)WAKILI DUNSTAN OMARI WAKIWAHUTUBIA WANAHABARI NJE YA MAHAKAMA YA MILIMANI 28/10/2022
Image: DOUGLAS OKIDDY

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amebanduliwa mamlakani,baada ya wabunge kupiga kura na kumtoa afisini.

Wabunge wa Bunge la Kaunti ya Meru waliwasilisha hoja ya kumtimua gavana huyo Jumatano asubuhi.

Hoja ya kumshtaki ilikamilika baada ya MCAs kuunga mkono kwa kiasi kikubwa.

Jumla ya MCAs 68 kati ya 69 walipiga kura ya kuunga mkono kuondolewa kwake.

MCAs wanamtaka aondoke afisini kwa madai ya utovu wa nidhamu, uteuzi wa mumewe katika afisi ya kaunti na madai ya kufutwa kazi kwa maafisa wa kaunti.

Wakati MCAs walipoanzisha mjadala wa kumshtaki Jumatano asubuhi, Mwangaza alikuwa amekataa kufika mbele ya Bunge kujitetea.

Gavana huyo alidai kuwa chaguo la MCAs kuwasilisha tena hoja ya kumtimua ni kudharau mahakama.

"Kuendelea na mchakato wa kumtimua itakuwa sawa na kuendeleza kwa ujanja uovu uliokusudiwa kuponywa na maagizo ya mahakama tukufu," alisema wakili wa Mwangaza Elias Mutuma.

Hoja ya kuondolewa  ilianzishwa mnamo Jumanne, Desemba 6, ambapo MCAs walimshtaki gavana huyo.