KCPE 2022: Fahamu jinsi ya kujua matokeo yako

Mtahiniwa anaweza kutumia huduma yoyote ya simu kuangalia matokeo yake.

Muhtasari

•Waziri alitangaza matokeo ya mtihani huo siku ya Jumatano adhuhuri baada ya kuyawasilisha kwa rais William Ruto.

•Mtihani wa KCPE 2022 ulifanywa kati ya Novemba 28 na Novemba 30 ambapo watahiniwa 1,244, 188 walijaribiwa.

wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC kando ya Barabara ya Dennis Pritt Kilimani, Nairobi mnamo Desemba 21, 2022.
Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi Belio Kipsang azungumza na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC kando ya Barabara ya Dennis Pritt Kilimani, Nairobi mnamo Desemba 21, 2022.
Image: ANDREW KASUKU

Watahiniwa wa KCPE 2022 sasa wanaweza kufahamu jinsi walivyofanya baada ya waziri Ezekiel Machogu kutangaza matokeo.

Waziri alitangaza matokeo ya mtihani huo siku ya Jumatano adhuhuri baada ya kuyawasilisha kwa rais William Ruto.

Watahiniwa wanaweza kujua matokeo yao kwa kutuma nambari yao ya usajili (Index Number)  kwa nambari 20076. Mtahiniwa anaweza kutumia huduma yoyote ya simu inayotumika hapa nchini kuangalia matokeo yake.

Mtihani wa KCPE 2022 ulifanywa kati ya Novemba 28 na Novemba 30 ambapo watahiniwa 1,244, 188 walijaribiwa.

Haya ni matokeo ya mtihani wa kitaifa ya kwanza kwa Machogu kutangaza baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa elimu takriban miezi miwili iliyopita. Pia ni matokeo ya kwanza katika utawala wa rais William Ruto.