Aliyekuwa waziri wa elimu George Magoha ameaga dunia

Kulingana na duru za habari Magoha aliaga kutokana na mshtuko wa moyo.

Muhtasari
  • Kifo chake kinakuja siku chache baada ya kumpoteza kaka yake. Ndugu huyo pia alikuwa profesa
George Magoha
George Magoha
Image: Maktaba

Aliyekuwa waziri wa elimu George Magoha ameaga dunia.

Waziri huyo wa zamani wa Elimu alifariki katika hospitali ya Nairobi siku ya Jumanne.

Kifo chake kinakuja siku chache baada ya kumpoteza kaka yake. Ndugu huyo pia alikuwa profesa.

Kulingana na duru za habari Magoha aliaga kutokana na mshtuko wa moyo.

Magoha alitambulika sana nchini katika juhudi zake za kubadilisha sekta ya elimu,huku akihudumu chini ya serikali ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Waziri huyo wa zamani wa elimu amefariki miezi 3 tu baada ya kuondoka ofisini.

Magoha ni nani

Prof Magoha ambaye ni mhitimu wa Shule ya Msingi ya DR Livingstone shule ya upili ya  wavulana ya Starehe,alihitimu kutoka Chuo cha Strathmore na Chuo Kikuu cha Lagos, Nigeria na Shahada ya Kwanza ya Udaktari.

Magoha alizaliwa mwaka wa 1952.